#HABARI: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imebaini kuwa idadi kubwa ya Wananchi Mkoani Dodoma, bado wanakabiliwa na uelewa mdogo wa haki zao za msingi, jambo linalochangia kuchelewa kupata haki au kufanyiwa uonevu katika jamii.
Akizungumza na waandishi wa Habari ikiwa ni siku ya 11 tangu kuanza kwa utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, Mchunguzi Mkuu Msaidizi wa THBUB, Bw. Halfan Botea, amesema Tume imejipanga vizuri kuhakikisha changamoto hiyo inapatiwa ufumbuzi.
Takwimu za Tume hiyo zinaonyesha kuwa changamoto kuu zinazowasumbua wananchi wa Dodoma ni pamoja na: Migogoro ya Ardhi, Uvamizi na dhuluma za maeneo ya ardhi, Mirathi na Ndoa, Ugomvi wa mali za marehemu, matunzo ya watoto, Ukiukwaji wa haki za wafanyakazi mahali pa kazi, Ukatili wa Kijinsia, na Mashauri yanayohusu ukatili ndani ya jamii.
Bwana Botea amesema Mbali na kupokea malalamiko, Tume imeweza kutoa elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa wananchi 69 waliofika bandani hapo.
Bw. Botea amebainisha kuwa wamebaini elimu ndogo kwa wananchi kuhusu haki za binadamu na utawala; wengi hawafahamu haki zao za msingi na hawajui mamlaka sahihi ya kushughulikia kero zao. Kupitia kampeni hii THBUB inatoa dira ili mwananchi ajue pa kwenda kuanzia ngazi ya kata hadi kitaifa.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inatoa fursa adhimu kwa wananchi kupata msaada wa kisheria bila malipo yoyote, lengo likiwa ni kurejesha misingi ya haki na utawala bora kwa kila Mtanzania.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)