Viongozi wa imani za dini walifanya maandamano ya amani ya Jumatatu ya Maadili (Moral Monday) nje ya Ikulu ya White House dhidi ya ‘vita visivyo vitakatifu’ katika eneo la Asia Magharibi.

Matakwa ya waandamanaji yalikuwa, hapana kwa vita, hapana kwa ukatili wa kisiasa, ndiyo kwa amani na ndiyo kwa haki.

Mchungaji Steven Tickner wa Kanisa Kuu la Kikristo la Marekani amesema katika maandamano hayo kwamba: Wanatumia mabilioni kwa mabilioni ya dola vitani, huku watu wengi hapa Marekani wakiteseka kutokana na ukosefu wa huduma za afya, ukosefu wa chakula, huduma za watoto na uhaba wa aina mbalimbali za vitu ambavyo tunapaswa kuwa navyo, lakini bado wanasema hatuwezi kumudu.

Mchungaji Steven Tickner ameongeza: Lakini bado wanaweza kumudu kwenda vitani na kutumia mabilioni ya dola.

“Hili si jambo takatifu. Ni utovu wa maadili. Maandiko yetu matakatifu katika Biblia ya Kikristo, ambayo ninawakilisha, yanapinga vita”, amesema Mchungaji Tickner.

Maandamano haya yamefanyika baada ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na CNN, kuonyesha kwamba asilimia 70 ya Wamarekani hawaridhishwi na utendaji wa kiuchumi wa Trump, ikiwa ni ishara ya wasiwasi mkubwa wa wapiga kura kuhusu hali ya kiuchumi ya nchi hiyo.

Wakati huo huo, mfumuko wa bei nchini Marekani uliongezeka kwa asilimia 3.8 mwezi Aprili 2026, kutokana na ongezeko la asilimia 17.9 la bei za nishati kutokana na vita kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran na kufungwa Mlango Bahari wa Hormuz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *