Wizara ya Ulinzi ya Iran imesema maadui, Marekani na Uzayuni, wanapaswa kukubali haki halali za taifa la Iran, au wasubiri kushindwa tena katika nyanja za kidiplomasia na katika uwanja wa vita.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Iran, Brigedia Jenerali Reza Talaei-Nik alitoa matamshi hayo Jumanne mjini Tehran.

“Bila kupata haki halali na za uhakika, adui hataweza kujinasua kutoka kwenye kinamasi alichonaswa ndani yake,” Talaei-Nik amesema.

Ameongeza kuwa Iran, ikiungwa mkono na mahudhurio ya watu wake uwanjani, imeonyesha uwezo wa juu katika mapambano na diplomasia.

“Ikiwa adui hatakubali matakwa halali ya Iran katika diplomasia, anapaswa kutarajia kushindwa tena katika uwanja wa kijeshi.”

Talaei-Nik amesema uwezekano wa kushindwa tena adui unatabirika kutokana na hali halisi katika eneo la Magharibi mwa Asia, na kwamba taifa la Iran litakuwa mshindi wa mwisho wa vita hivi vya kulazimishwa.

Vilevile amesema tishio lolote jipya, uchokozi au ukiukaji wa sheria wa adui utakabiliwa na jibu kali, la mwisho na la kujutisha.

“Kukimbia mara kwa mara kwa meli za kijeshi za Marekani kutoka eneo la mzozo kunaonyesha azma na uwezo wa vikosi vya jeshi la nchi yetu, na tuko tayari kikamilifu kutoa jibu la kujutisha kwa uchokozi wa aina yoyote,” amesema Brigedia Jenerali Reza Talaei-Nik.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *