Waziri wa zamani wa nishati nchini Nigeria Saleh Mamman, amehukumiwa jela miaka 75, baada ya kupatikana na hatia ya kuiba mabilioni ya Dola kutoka kwenye miradi ya taifa ya kuzalisha umeme.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mahakama inayoshughulikia maswala ya uhalifu wa kiuchumi jijini Abuja, imempata na hatia Waziri huyo wa zamani kwa kuiba fedha za umma, Naira Bilioni 33.8 sawa na Dola Milioni 24.6.

Jaji James Omotosho katika ukurasa wa kijamii wa X, ameandika uamuzi huo, akieleza kuwa Mahakama imebaini pasipo shaka kuwa Waziri huyo wa zamani alilangua fedha hizo zilizopaswa kuimarisha na kusaidia upatikanaji wa umeme nchini Nigeria.

Waziri huyo wa zamani, alitumika serikalini kati ya mwaka 2019 na 2021 wakati wa utawala wa aliyekuwa rais Marehemu Muhammadu Buhari na hukumu yake ilitolewa bila ya uwepo wake Mahakamani.

Anakuwa Waziri wa kwanza chini ya utawala wa Buhari kufunguliwa mashtaka na kupatikana na hatia ya ufisadi, huku kesi za waliokuwa Mawaziri wa Sheria na kazi zikiendelea, akiwemo Gavana wa zamani wa Benki Kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *