Wiki mbili za mapigano makali nchini Sudan Kusini zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 61, wakiwemo watoto tisa, kundi la madaktari wa eneo hilo limetangaza siku ya  Jumatano. Mapigano haya ni sehemu ya vita kubwa zaidi ambayo imeikumba nchi hiyo tangu mwaka 2023.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Mtandao wa Madaktari wa Sudan, unaofuatilia waathiriwa wa mzozo huo, mapigano hayo yalizuka mapema mwezi huu kati ya vikosi vinavyohusishwa na kundi la Ukombozi wa Watu wa Sudan-Kaskazini (SPLM-N) na kabila la Otoro katika mji wa Kauda, ​​​​Kordofan Kusini.

Vita vya Sudan ambavyo sasa viko katika mwaka wake wa nne , vimesababisha nchi hiyo kugawika ambapo jeshi linadhibiti maeneo ya kaskazini, mashariki na kati yenye mabomba na makampuni ya kusafisha mafuta, huku kundi la RSF na washirika wake wakidhibiti eneo la magharibi mwa Darfur na Kordofan, maeneo yenye utajiri wa mafuta na migodi ya dhahabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *