China imetaka mapigano yasitishwe kabisa Mashariki ya Kati na kufunguliwa tena kwa Lango la Hormuz “haraka iwezekanavyo,” pembezoni mwa mkutano kati ya Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Marekani Donald Trump huko Beijing, leo Ijumaa, Mei 15,.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Njia za baharini lazima zifunguliwe tena haraka iwezekanavyo, kama inavyotakiwa na jumuiya ya kimataifa… Usitishaji mapigano kamili na wa kudumu lazima uanzishwe haraka iwezekanavyo,” Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema katika taarifa leo Ijumaa. “Vita hivi, ambavyo havikupaswa kutokea kamwe, havina sababu ya kuendelea.”

Siku ya Alhamisi, Mei 14, shirika la habari la Iran la Tasnim lilitangaza kwamba vikosi vya majini vya Iran vimeruhusu “meli kadhaa” za China kupita katika Mlango-Bahari wa Hormuz siku iliyotangulia.

Katika ziara rasmi nchini China, rais wa Marekani alisemasiku ya  Alhamisi kwamba mwenzake wa China alimhakikishia kwamba Beijing “haitatoa vifaa vya kijeshi” kwa Tehran. Katika mahojiano na Fox News, Donald Trump pia alisema kwamba Xi Jinping alitaka “kuona Mlango-Bahari wa Hormuz ukifunguliwa”: “Alisema, ‘Kama naweza kusaidia, ningefurahi kusaidia.'”

Iran “inapaswa” kufikia makubaliano, anaonya Donald Trump

Rais wa Marekani alionya Iran kwamba inahitaji kufikia makubaliano na Marekani, miezi miwili na nusu baada ya kuanza kwa vita katika Mashariki ya Kati na wakati makubaliano ya kusitisha mapigano yakiendelea.

“Sitakuwa na subira zaidi (…) Wanapaswa kufikia makubaliano,” Donald Trump alisema katika mahojiano yaliyorushwa siku ya Alhamisi na Fox News.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *