Israel na Lebanon zakubaliana kuongeza muda wa usitishaji mapigano kwa siku 45Israel na Lebanon zakubaliana kuongeza muda wa usitishaji mapigano kwa siku 45

Bendera ya Israel na Lebanon

Chanzo cha picha, Getty Images

Lebanon imekaribisha makubaliano na Israel ya kuongeza muda wa
usitishaji mapigano kwa siku 45, ambao ulikuwa unatarajiwa kumalizika siku ya Jumapili,baada ya mazungumzo yaliyofanyika Marekani mwezi Aprili.

Hata hivyo, vikosi vya Israel vilishambulia miji na
vijiji vya kusini mwa Lebanon, na kuua angalau watu 12 siku ya Ijumaa, wakiwemo
wahudumu watatu wa afya.

Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni wa Marekani, Tommy Pigott, alisema kuwa “Tunatumai mazungumzo haya yatachangia katika kupatikana kwa amani ya kudumu kati ya nchi hizo mbili, kutambuliwa kikamilifu kwa mamlaka na mipaka ya kila upande, pamoja na kuimarishwa kwa usalama katika mpaka wa mataifa hayo.”

Pia unaweza kusoma:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *