
Kiongozi wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la Islamic State ameuawa katika oparesheni ya pamoja na jeshi la Marekani na Nigeria Magharibi ya taifa hilo la Afrika Magharibi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Abu-Bilal al-Minuki alitangaziwa vikwazo na Marekani mwaka wa 2023 na amekuwa akihudumu katika nafasi ya naibu kiongozi wa kundi la IS kote duniani.
Rais wa Marekani Donald Trump kupitia mtandao wake wa kijamii wa Truth Social amesema aliwaagiza wanajeshi wa nchi yake kutekeleza oparesheni dhidi ya al-Minuki.
Jeshi la Nigeria nalo limesema al -Minuki alikuwa gaidi mkubwa zaidi duniani, na alikuwa akitoa maelekezo kwa magaidi wa kundi la ISIS nje ya Nigeria haswa katika masuala ya utegenezaji wa silaha, vilipuzi na droni.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu amesema Al-Minuki, maarufu kama Abu-Mainok, aliuawa pamoja na wapiganaji wengine wakati wa shambulio dhidi ya makazi yake katika eneo la Lake Chad Basin”, eneo la mpaka kati ya Niger, Chad and Cameroon.
