Rwanda: Felicien Kabuga, mshukiwa wa mauaji ya kimbari ameaga duniaRwanda: Felicien Kabuga, mshukiwa wa mauaji ya kimbari ameaga dunia

Felicien Kabuga, 93, mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 nchini Rwanda, ameaga dunia wakati akiwa kizuizini kulingana na taarifa ya mahakama ya Umoja wa Mataifa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kabuga alikamatwa nchini Ufaransa mwaka wa 2020 baada ya kuwa mafichoni kwa kipindi kirefu na kusafirishwa hadi katika mahakama ya The Hague.

Mahakama baadaye iliagiza kuwa hangeweza kuendelea na kesi dhidi yake kutokana na afya yake kuwa mbaya na pia hangesafirishwa kwenda Rwanda.

Baada ya kukataliwa na kila nchi, Kabuga alisalia katika kizuizi cha Umoja wa Mataifa jijini The Hague. ​Mahakama imesema imeanzisha uchunguzi kubaini mazingira ya kifo chake.

Kabuga mfanyibiashara wa zamani na mmiliki wa kituo cha redio alikuwa miongoni mwa washukiwa wa mwisho waliokuwa wakitafutwa kwa mchango wao katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda. Watusi Laki nane waliuawa wakati huo wa mapigano ya siku 100.

Waendesha mashataka wa ICC walimtuhumu Kabuga kwa kuchochea chuki kupitia kwenye radio na televisheni ya Libre des Mille Collines pamoja na kusaidia kuwahami wahutu wenye silaha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *