Che Malone apooza machungu USMA ikitwaa Kombe la Shirikisho AfrikaChe Malone apooza machungu USMA ikitwaa Kombe la Shirikisho Afrika

Beki wa zamani wa Simba, Che Fondoh Malone amevaa medali ya dhahabu ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya timu yake ya USMA ya Algeria kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 8-7 dhidi ya Zamalek ya Misri katika mechi ya pili ya Fainali ya mashindano hayo iliyochezwa leo Jumamosi, Mei 16, 2026 jijini Cairo, Misri.

Kutwaa taji hilo hapana shaka kumemfuta machozi Che Malone ambaye msimu uliopita, alipoteza fainali ya mashindano hayo akiwa na Simba.

Beki wa USM Alger, Che Malone wakati akiwa amebeba Kombe la Shirikisho Afrika ambalo amefanikiwa kutwaa baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Zamaleki.

Katika mchezo wa leo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, dakika 90 zilimalizika kwa ushindi wa bao 1-0 ambao wenyeji Zamalek waliupata kupitia bao la mkwaju wa penalti wa Oday Dabbagh.

USMA waliweza kujilinda vyema hadi dakika 90 zilipomalizika na hivyo kufanya mshindi wa hatua ya fainali kupatikana kwa mikwaju ya penalti kutokana na matokeo ya mechi mbili baina yao kuwa sare ya bao 1-1 kwa vile USMA walishinda bao 1-0 katika mechi ya kwanza wiki iliyopita nchini Algeria.

Baadhi ya wachezaji  wa USM Alger, wakiwa wanashangilia baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika ambalo baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Zamaleki.

Baada ya kila timu kufunga penalti saba, Mohamed Shehata wa Zamalek alipoteza penalti yake kisha Glody Likonza akafunga ya USMA na kuihakikishia taji hilo.

Kwa kutwaa ubingwa huo, USMA imejihakikishia kitita cha Dola 4 milioni (Sh10.5 bilioni) kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF). Zamalek imepata kitita cha Dola 1 milioni (Sh2.6 bilioni)

Hii ni mara ya pili kwa USMA kutwaa taji hilo ambapo mara ya kwanza ilifanya hivyo msimu wa 2022/2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *