Watendaji wa serikali wanaosimamia miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi wamekutanishwa katika mafunzo maalum kwa lengo la kupigwa msasa na kuimarishwa uwezo wao katika uibuaji, uchambuzi na usimamizi wa miradi hiyo nchini.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Kituo cha PPP yamewaleta pamoja maafisa kutoka serikali kuu, mamlaka za serikali za mitaa pamoja na wadau wa sekta binafsi, yakilenga kuwajengea uelewa wa kina kuhusu taratibu, majukumu ya kisheria na utekelezaji bora wa miradi ya ubia.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Maandalizi na Uchambuzi wa Miradi ya PPP, Augustino Saibull, amesema mafunzo hayo yanawasaidia watendaji kufahamu hatua zote muhimu kuanzia uibuaji wa miradi, maandalizi, ununuzi hadi usimamizi wake, ili kuhakikisha miradi inayowasilishwa inakidhi vigezo na kutoa tija kwa taifa.
Saibull ameongeza kuwa mafunzo hayo ni ya lazima na endelevu, akisisitiza kuwa mabadiliko ya sheria na mazingira ya biashara yanahitaji watendaji kuwa na uelewa wa kisasa ili kuongeza uwazi, ufanisi na kuondoa urasimu usio wa lazima katika utekelezaji wa miradi ya PPP.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)
