Wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Geita wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DktWachimbaji wadogo wa madini Mkoani Geita wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt

Wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Geita wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake kubwa za kuimarisha sekta ya madini nchini, hatua inayozidi kuwainua wachimbaji wadogo na kuleta matumaini mapya kwa vijana wengi wanaotegemea sekta hiyo kujikwamua kiuchumi.

Kupitia sera zake rafiki kwa wawekezaji na wachimbaji wa ndani, maeneo mengi ya uchimbaji sasa yamekuwa na mazingira bora zaidi ya kazi na uzalishaji, Vijana Mkoani Geita wakimshukuru kwa kuwaongezea thamani kupitia mabadiliko makubwa ya sera na uwezeshaji wa serikali kupitia Vyama vya ushirika ambavyo vimesababisha Vijana wengi kuweza kuingia katika uchimbaji wa madini.

Katika Mkoa wa Geita kupitia kikundi cha Mgusu Miners, vijana wanaojishughulisha na uchimbaji madini wameeleza kufurahishwa na namna serikali ya awamu ya sita ilivyoleta mageuzi makubwa katika shughuli za uchimbaji madini, ikiwemo kuboresha miundombinu, kutoa elimu kwa wachimbaji pamoja na kuongeza usimamizi wenye tija. Wamesema hatua hizo zimeongeza mapato kwa wachimbaji na kuchochea ukuaji wa uchumi wa maeneo yao.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *