Wizara ya Uchukuzi imesema maandalizi ya kuanza kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Bahi mkoani Dodoma kwa…Wizara ya Uchukuzi imesema maandalizi ya kuanza kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Bahi mkoani Dodoma kwa…

Wizara ya Uchukuzi imesema maandalizi ya kuanza kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Bahi mkoani Dodoma kwa kutumia reli yako katika hatua za mwisho, hatua inayolenga kupunguza msongamano bandarini na kero ya foleni.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Godius Kahyarara, amesema utayari wa Shirika la Reli Tanzania, TRC, ni suluhisho la changamoto ya muda mrefu ya uhifadhi wa mizigo bandarini, akibainisha kuwa tatizo si wingi wa mizigo bali ni mahali pa kuihifadhi.

Amesema huduma hiyo itakapokamilika itaboresha ufanisi wa usafirishaji wa mizigo na kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *