
Marekani imetangaza Jumatatu, Mei 18, 2026, udhibiti mkali kwenye mipaka yake ili kupambana na virusi vya Ebola, ambavyo vimemwambukiza raia wa Marekani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), idara kuu ya afya ya umma nchini Marekani, vilitangaza utekelezaji wa vikwazo vya kuingia kwa raia wa kigeni wanaowasili kutoka maeneo yaliyoathiriwa na virusi vya Ebola barani Afrika.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangazo kuu la CDC ni kizuizi cha kuingia Marekani kwa raia yeyote wa kigeni ambaye amesafiri katika siku 21 zilizopita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, au Sudan Kusini. Hatua hii ya dharura ya shirika la afya la Marekani inafuatia maambukizi ya Ebola ya raia wa Marekani ambaye alipimwa na kupatikana na virusi siku mbili zilizopita na anakaribia kuhamishiwa hospitali ya kijeshi ya Marekani nchini Ujerumani.
Daktari katika Hospitali ya Nyankunde
Huyu ni daktari wa Marekani kutoka shirika la kibinadamu la Kikristo Serge, ambaye amekuwa katika kazi kwa miaka mitatu katika Hospitali ya Nyankunde, iliyoko kilomita 45 kusini magharibi mwa Bunia, anaripoti mwandishi wetu huko Kinshasa, Pascal Mulegwa. Inaaminika alipata virusi hivyo alipokuwa akiwatibu wagonjwa hospitalini. Mkewe na jamaa mwingine wa karibu, wote Wamarekani, bado hawana dalili na wamewekwa karantini.
Watu wengine sita, ambao uraia wao haujatajwa, pia wanatarajiwa kurejeshwa Ujerumani hivi karibuni. Kulingana na tovuti ya habari ya Marekani Stat, hawa wanaweza pia kuwa Wamarekani waliopo katika eneo hilo kwa sasa.
Hii si mara ya kwanza Ujerumani kupokea Wamarekani walioambukizwa virusi vya Ebola, anabainisha mwandishi wetu huko Berlin, Nathalie Versieux. Mnamo mwaka 2014, wanajrshi kadhaa wanaoshukiwa kuambukizwa virusi hivyo waliwekwa karantini katika kituo cha kijeshi cha Baumhold magharibi mwa DRC. Kitengo hiki chenye usalama wa hali ya juu kina takriban vitanda 180 vilivyotengwa. Askari wenye homa walitumwa moja kwa moja katika Hospitali ya Jeshi ya Landstuhl, hospitali kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani nje ya Marekani.
Hatari ndogo kwa raia wa Marekani
Mbali na uchunguzi wa afya kwa wasafiri kutoka maeneo yaliyoathiriwa, Washington itazuia kwa muda utoaji wa visa katika nchi husika. Hatua hii tayari inatumika katika Ubalozi wa Marekani jijini Kampala.
Ingawa Idara ya afya ya Marekani inabainisha kuwa inafanya kazi ya kuwarudisha nyumbani “idadi ndogo ya raia wake walioathiriwa moja kwa moja na mlipuko huo,” inaamini hatari ya haraka kwa idadi ya watu wa Marekani bado ni ndogo. Kama ukumbusho, WHO ilitangaza mlipuko wa Ebola nchini DRC kuwa Dharura ya Afya ya Umma inayotia wasiwasi Kimataifa.
