Tanzania: Tume maalum yauundwa kuchunguza vurugu za baada ya uchaguziTanzania: Tume maalum yauundwa kuchunguza vurugu za baada ya uchaguzi

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuunda tume nyingine maalumu ya jinai itakayochunguza matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka jana.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangazo la kuundwa kwa tume hii linakuja majuma kadhaa kupita tangu tume ya awali iliyochunguza yaliyotokea wakati wa uchaguzi, kupendekeza serikali kuunda tume ya jinai kubaini vitendo vilivyofanyika na wahusika kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na katibu mkuu kiongozi, tume hiyo imeundwa kwa mujibu wa sheria na kwamba itakuwa na jukumu la kubaini ukweli kuhusu matukio ya vurugu, mauaji na vitendo vingine vyenye utata wakati wa uchaguzi huo.

Serikali inasema tume hiyo itakayoongozwa na jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa Shaban Lila, inatarajiwa kufanya uchunguzi wa kina na kupendekeza hatua za kisheria na kiungozi zinazopaswa kuchukuliwa.

Tume hii imetangazwa wakati huu ripoti ya tume ya awali ikikataliwa na baadhi ya mashirika ya kutetea haki za binadamu pamoja na vyama vya upinzani, ambao wanadai haikufanya kazi yake ilivyotarajiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *