Ebola nchini DRC: Kuanzia Mongbwalu hadi Bunia, jinsi mwitikio dhidi ya virusi unavyopangwaEbola nchini DRC: Kuanzia Mongbwalu hadi Bunia, jinsi mwitikio dhidi ya virusi unavyopangwa

Wakazi wa mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameanza miongozi ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Ebola. Mkoa huu wa kaskazini mashariki ndio kitovu cha mlipuko huo. Ni katka mkoa huu ndipo visa vya kwanza viliripotiwa wiki iliyopita, hasa katika maeneo ya migodi ya Mongbwalu na Rwampara.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mashariki mwa DRC, mlipuko mpya wa Ebola umeikumba Mongbwalu, mji wa madini katika jimbo la Ituri. Ni mji unaotembelewa kila siku na wafanyabiashara, wachimba migodi wadogo, na wasafirishaji. Lakini nyuma ya takwimu rasmi, ukweli uliopo unaendelea kuwa wa kutisha sana.

Huko Mongbwalu, hospitali kuu tayari inafanya kazi chini ya shinikizo kubwa. “Hakuna vitanda vya kutosha vya kuwahudumia wagonjwa,” anasema Jonathan Imbalapay, kiongozi wa shirika la kiraia la Mongbwalu, ambaye ameshuhudia hali hiyo ikizidi kuwa mbaya katika wiki za hivi karibuni. “Tunaposema hospitali imejaa, inamaanisha hakuna vitanda vya kutosha. Baadhi ya wagonjwa wanalala sakafuni, na bado tunajitahidi kutumia rasilimali za ndani,” anabainisha.

Mojawapo ya changamoto za dharura zaidi sasa ni kuwatenganisha wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Ebola na wagonjwa wengine wanaotibiwa hospitalini. Zaidi ya watu ishirini kwa sasa wako peke yao, kulingana na mamlaka za eneo hilo. Lakini vituo maalum havipo. “Tayari tumebaini eneo. Ardhi imesawazishwa na kampuni ya uchimbaji madini. Sasa kilichobaki ni ujenzi,” anasema Israel Sesereki Mandro, meya wa wa mji wa Mongbwalu.

Wakati huo huo, washirika wa kwanza wa kibinadamu wanawasili hatu kwa hatua. Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) wanapeleka vifaa vya utabibu wa dharura. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) pia limewasili tu katika wilaya. Lakini kupeleka vifaa katika eneo hilo haraka bado ni ngumu: uwanja wa ndege wa Mongbwalu haufanyi kazi.

Kwa hivyo, wakati huo huo, raia wanajaribu wenyewe kukabilina na hali hiyo. Katika masoko, shule, na maduka, vituo vya kunawa mikono vinaonekana kila mahali. Wauzaji wa maduka wanaweka vifaa vyao wenyewe. “Kuna ukosefu wa vituo vya kunawa mikono sokoni, barakoa, dawa, vitu kama hivyo,” anasema Israel Sesereki Mandro.

Mashirika ya kiraia sasa yanaomba uhamasishaji mkubwa kutoka kwa mamlaka za kitaifa: “Tunaomba mamlaka kuingilia kati haraka. Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola si hali ya kuchukuliwa kirahisi. Lazima watusaidie,” anaomba Jonathan Imbalapay.

Na licha ya mlipuko huo, jiji linaendelea kufanya kazi. Shule na masoko yanaendelea kuwa wazi. Shughuli za uchimbaji madini zinaendelea pia. Wakazi wanaendelea kusafiri hadi Bunia na Kivu Kaskazini. Mashirika ya kiraia yanaelezea raia ambao wana wasiwasi na msongo wa mawazo, lakini ambao polepole wanaanza kuchukulia ugonjwa huo kwa uzito baada ya wiki kadhaa za uvumi na imani za kishirikina zinazozunguka vifo vya kwanza.

Miongozo imechukuliwa kwa umakini huko Bunia

Huko Bunia, mji mkuu wa mkoa, zaidi ya tani 16 za vifaa na dawa zilizokusudiwa kwa ajili ya kukabiliana ziliwasilish siku ya Jumanne na serikali ya mkoa. Tangu siku ya Jumatatu, vituo mbalimbali vya redio vya jiji vimekuwa vikirusha jumbe za uhamasishaji kwa lugha ya wenyeji: “Osha mikono yako, vaa barakoa, epuka kushikana mikono.” “Watu wanachukulia maagizo haya kwa umakini sana,” anaeleza mkazi mmoja, ambaye anasema kwamba zaidi ya nusu ya watu mitaani wamevaa barakoa, wakiwemo madereva wa pikipiki, anaongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *