Jeshi la Iran: Medani mpya za mapambano zitafunguliwa ikiwa adui atatumbukia katika mtego wa IsraelJeshi la Iran: Medani mpya za mapambano zitafunguliwa ikiwa adui atatumbukia katika mtego wa Israel

Jeshi la Iran limeonya kuwa iwapo adui ataanguka tena katika mtego wa Israel na kuanzisha uchokozi mwingine dhidi ya Iran, jeshi la taifa litafungua medani mpya ya mapambano kwa kutumia zana na mbinu mpya.

Brigedia Jenerali Mohammad Akraminia, Msemaji wa Jeshi la Iran amesema haya katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Valiasr mjini Tehran.

“Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haiwezi kuzingirwa au kupata kipigo”, ameongeza kusema Jenerali Akraminia.

” Iwapo adui atathubutu kufanya upumbavu mwingine na kuanguka tena kwenye mtego wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kuanzisha tena uchokozi mwingine dhidi ya nchi yetu pendwa, tutafungua medani mpya kwa kutumia zana na mbinu mpya,” amesema msemaji wa Jeshi la Iran.

Brigedia Jenerali Mohammad Akraminia pia amewasilisha ripoti kuhusu hatua zilizpchukuliwa na vikosi vya ulinzi vya Iran na kusema: Jeshi limetumia kipindi cha usitishaji vita kama fursa kuimarisha nguvu zake za makabiliano vitani.

Brigedia Jenerali Akraminia amesema: Vikosi vya ulinzi vya Iran vinadhibiti kikamilifu Mlango-Bahari wa Hormuz, na kwamba hali ya mambo katika njia hiyo ya kimkakati ya majini haitarejea katika hali yake ya awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *