Zaidi ya wakazi elfu tatu manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA mkoa wa Shinyanga ambapo imeelezwa kuwa uelewa mdogo wawananchi juu ya masuala ya vitambulisho vya Taifa NIDA ni sababu ya wananchi wengi kushindwa kufuatilia mchakato wa kupata vutambulisho hivyo nakusubiri hadi wanapopatwa na changamoto inayowalazimu kuwa na vitambulisho ivyo.
Asifa usajili NIDA mkoa wa Shinyanga Devotha Nchia amebainisha hayo katika kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid awamu ya pili mkoa wa Shinyanga ambapo amesema kuwa kampeni hiyo imerahisisha kuwafikia watu wengi zaidi tofauti na huduma hizo zinapotolewa ofisini.
Aidha amesema kuwa mamlaka hiyo imeandaa utaratibu wa kuwafikia wananchi katika kata zao kwa ajili ya ugawaji wa vitambulisho vya NIDA katika maeneo waliyojiandikisha badala ya kufika ofisini.
baadhi ya wananchi waliofika kupata huduma katika kampeni hiyo wamefurahishwa utaratibu wa utoaji huduma ambao hauna mtiririko mrefu wa kuonana na wataalamu ukilinganisha na huduma zinazotolewa ofisini.
(Feed generated with FetchRSS)
