Aston Villa yaipeleka Bournemouth Ligi ya Mabingwa UlayaAston Villa yaipeleka Bournemouth Ligi ya Mabingwa Ulaya

AFC Bournemouth imeandika historia mpya baada ya kujihakikishia nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake miaka 147 iliyopita.

Mafanikio hayo yamekuja baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Manchester City katika mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Mei 19, 2026 lakini mafanikio ya Aston Villa kutwaa ubingwa wa Europa League kwa kuichapa Freiburg mabao 3-0 umeihakikishia Bournemouth tiketi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Awali, Bournemouth ilikuwa imehakikisha nafasi ya kushiriki mashindano ya Europa League, lakini ushindi wa Aston Villa umebadilisha kabisa mwelekeo wao katika michuano ya Ulaya msimu ujao.

Wachezaji wa Aston Villa wakati wakishangilia ubingwa wa Kombe la Europa League baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Freiburg, Mei 20, 2026. Picha na Mtandao

Villa, ambao wametwaa Kombe la Europa League huku pia wakimaliza katika nafasi zinazowapa tiketi ya Ligi ya Mabingwa kupitia msimamo wa Ligi Kuu England, wameifanya England kupata nafasi ya ziada ya kushiriki michuano hiyo ya Ulaya kwani wao watashiriki michuano hiyo kwa tiketi ya ubingwa wa Kombe la Europa.

Hali hiyo imeifanya Bournemouth kupanda rasmi na kujihakikishia nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, mafanikio yanayotajwa kuwa makubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *