Mbunge wa Geita Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chacha Wambura, amesema changamoto kubwa inayowakabili wananchi katika …Mbunge wa Geita Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chacha Wambura, amesema changamoto kubwa inayowakabili wananchi katika …

Mbunge wa Geita Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chacha Wambura, amesema changamoto kubwa inayowakabili wananchi katika maeneo mengi nchini ni ubovu wa miundombinu ya barabara zinazohudumiwa na TARURA na TANROADS.

Akizungumza bungeni, mbunge huyo amesema mahitaji ya maendeleo ni makubwa kuliko uwezo wa bajeti iliyopo. Hali hiyo, amesema, imekuwa sababu ya baadhi ya miradi ya maendeleo kushindwa kutekelezwa kwa wakati.

Amesema ili nchi iweze kuboresha miundombinu kwa kiwango kinachohitajika, Serikali inapaswa kuongeza vyanzo vya mapato ya ndani.

Pia ameshauri kufanyika kwa maboresho katika sekta zinazokusanya fedha nyingi ikiwemo bandari na maeneo mengine ya kimkakati.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, maendeleo ya barabara hayawezi kupatikana bila uwepo wa fedha za kutosha.

Hivyo, amewataka Watanzania kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Aidha, amekiri kuwa baadhi ya hatua za kuongeza mapato zinaweza kuwa na changamoto kwa wananchi kwa muda mfupi.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa ni muhimu taifa kuweka mbele maslahi ya maendeleo ya baadaye na kujitegemea katika kutatua changamoto zake za maendeleo.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *