Putin wa Russia na Xi wa China walaani kwa pamoja vita vya uchokozi vya Marekani na Israel dhidi ya IranPutin wa Russia na Xi wa China walaani kwa pamoja vita vya uchokozi vya Marekani na Israel dhidi ya Iran

Rais wa Russia, Vladimir Putin, na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping, wamekemea kwa pamoja vita vya hivi karibuni vya uchokozi vilivyoanzishwa na Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wakisisitiza kwamba njia pekee ya kumaliza mzozo huo unaotishia uthabiti wa kanda ni kupitia mazungumzo na diplomasia.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumatano, wakati Putin akiwa katika ziara rasmi nchini China, viongozi hao wawili walieleza makubaliano yao kwamba mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran yanakiuka sheria za kimataifa na misingi ya kimsingi ya mahusiano ya kimataifa, na kwamba yameathiri vibaya uthabiti wa eneo la Asia Magharibi.

Putin na Xi walisisitiza umuhimu wa pande husika kurejea haraka katika mazungumzo na majadiliano ya kidiplomasia, kwa lengo la kuzuia kuenea zaidi kwa mzozo huo. Aidha, wameitaka jamii ya kimataifa kuchukua msimamo wa haki na usioegemea upande wowote, kusaidia kupunguza mvutano katika eneo la Asia Magharibi, na kulinda kwa pamoja kanuni za msingi za mahusiano ya kimataifa.

Marekani, kwa ushirikiano wa karibu na utawala katili wa Israel, ilianzisha vita dhidi ya Iran tarehe 28 Februari bila uchokozi wowote kutoka upande wa Iran, hatua iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 3,300 na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya kiraia.

Kwa kujibu mashambulizi hayo, majeshi ya Jamhuri ya Kiislamu yalifanya operesheni za kila siku za makombora na ndege zisizo na rubani, zikilenga maeneo katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel pamoja na kambi na vituo vya kijeshi vya Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *