
Akijibu uchokozi na ukiukwaji wa mapigano uliofanywa na Marekani, Spika wa Bunge la Iran amesisitiza kuwa: “Ukivunja ahadi na majukumu yako, tutatumia lugha tunayoijua vyema.”
Mohammad Baqer Qalibaf, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge), ameandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa X kwamba: “Tunapendelea lugha ya diplomasia, lakini tunazungumza lugha zingine kwa ufasaha zaidi.”
Spika wa Bunge la Iran ameongeza: “Ukivunja ahadi na majukumu yako, tutatumia lugha tunayoijua vyema. Utapanda farasi yuleyule uliyemuwekea tandiko!”
Itakumbukwa kuwa mapema leo, maeneo manne muhimu katika kambi ya anga na kituo cha amri na udhibiti cha jeshi la mauaji ya watoto la Marekani huko Al-Azraq, Jordan yameshambuliwa kwa makombora ya Jeshi la Walinzi wa Jamhuri ya Kiislamu (IRGC).
Taarifa ya IRGC imesema vikosi vya Jeshi la Uislamu na wapiganaji shupavu wa Kikosi cha Anga cha IRGC wamepiga na kuharibu malengo 4 muhimu, ikiwa ni pamoja na hangari za ndege za kivita za F35 kwenye kambi ya anga na kituo cha amri na udhibiti cha jeshi la mauaji ya watoto la Marekani huko Al-Azraq, nchini Jordan, kwa makombora ya fueli mango ya masafa marefu.
Taarifa ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambayo imeanza kwa Aya ya 194 ya Suratul Baqara inayosema: “Na anayekushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyokuchokozeni”, imesema: Vikosi vyetu viko tayari kutoa majibu makali zaidi kwa uchokozi wowote mpya kutoka kwa adui, na matokeo ya uchokozi mpya yatakuwa jukumu la adui Mmarekani.
Saa nane na nusu usiku wa kuamkia leo pia, Jeshi la Wanamaji la IRGC lilifanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye makao makuu ya Kikosi cha Tano cha Wanamaji cha jesi la Marekani nchini Bahrain na katika ambi ya jeshi la Marekani ya Ali al Salem huko Kuwait.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limefanya mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi baada ya Marekani kushambulia maeneo kadhaa katika Mkoa wa Hormozgan, kusini mwa Iran.