Maandamano yafanyika Dublin kulaani mauaji ya raia wa DRCMaandamano yafanyika Dublin kulaani mauaji ya raia wa DRC

Mamia ya wandamanaji walijitokeza hapo jana nje ya bunge la Ireland kulalamikia kifo cha raia wa DRC akiwa mikononi mwa maofisa wa usalama wiki iliopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Yves Sakila alizuiliwa na maofisa wa usalama jijini Dublin Mei 15 kwa tuhuma za kuiba kwenye duka moja na kisha kutangazwa kuaga dunia kwenye eneo la tukio.

Kulingana na video ya tukio hilo iliyosambaa mtandaoni, Sakila anaonekana akiwa kwenye sakafu wakati wanaume watano wakiwa wamembana juu ya mgongo kwa karibia dakika tano wakati watu wakitazama.

Tukio hilo limeibua kumbukumbu ya mauaji ya raia mweusi wa Marekani, George Floyd, aliyeuwa na maofisa wa polisi jijini Minneapolis mwaka wa 2020.

Mamlaka nchini Ireland imesema imeanzisha uchunguzi kwenye tukio hilo.
Mamlaka nchini Ireland imesema imeanzisha uchunguzi kwenye tukio hilo. REUTERS – NATALIA CAMPOS

Wanaume wawili wanaonekana wakiwa wamemkaba uso wake wakati akiwa sakafuni, mmoja wa wanaume hao wakati mmoja akionekana kuweka mguu wake kwenye Shingo ya Sakila kwa sekunde kadhaa.

Waandamanaji hao sasa wanashinikiza haki kutendeka kwa Yves Sakila. 

Polisi nchini Ireland wamesema wanaendelea na uchunguzi kubaini kilichotokea na kuwawajibisha waliohusika na mauaji hao.

Waziri Mkuu wa Ireland   Micheal Martin naye ametoa wito wa uchunguzi kufanyika katika tukio hilo ambalo limewashangaza watu wengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *