Ebola DRC: Hospitali ya CBCA Virunga Goma inajaribu kurekebisha vituo vyake vya afyaEbola DRC: Hospitali ya CBCA Virunga Goma inajaribu kurekebisha vituo vyake vya afya

Kwa usaidizi wa Shirika lisilo la kiserikali la Medical Corps, taasisi hiyo katika mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini unayodhibitiwa na wasi wa AFC/M23 imeanzisha mzunguko mpya wa kuwapima wagonjwa na kuwaweka karantini wagonjwa wanaoonyesha dalili za maambukizi ya virusi vya Ebola.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini unaodhibitiwa na waasi wa AFC/M23, ambapo kisa cha Ebola kimerekodiwa, juhudi za kurekebisha vituo vya afya ili kudhibiti ugonjwa huo zinaongezeka. Kwa usaidizi kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Medical Corps (IMC), hospitali ya CBCA Virunga sasa ina, miongoni mwa mambo mengine, mfumo mpya wa upimaji na utenganishaji kwa wagonjwa wanaoshukiwa kuwa kuambikizwa virisi vya Ebola.

Wakati wa kuingia katika kituo hicho, kila mgonjwa mpya lazima sasa aoshe mikono yake na kupimwa joto. “Kila mgonjwa anayefika hufanyiwa uchunguzi. Ikiwa ana homa, basi huelekezwa kwenye eneo la upimaji, iwe ni mgonjwa au la,” anaeleza Dieudonné Igunzi, muuguzi katika hospitali hiyo.

Wagonjwa wanaoonyesha dalili za Ebola kisha huingizwa moja kwa moja katika wodi za wagonjwa waliowekwa karantini zinazosimamiwa na Shirika lisilo la kiserikali la IMC. “Tunawapima wagonjwa kulingana na dalili zao. Visa ambavyo havifikii vigezo vya ugonjwa wa virusi vya Ebola huelekezwa kwenye eneo safi. Tangu tulipofika, wagonjwa kumi na moja wametumwa kwetu. Lakini, hadi sasa, hakujawa na wagonjwa wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola,” anaeleza Tabuley Lesumbe, mwanachama wa IMC.

Katika kituo cha wagonjwa waliowekwa karantini, vitanda vimewekwa katika kila chumba ili kuzuia mawasiliano au kutangamana kati ya wagonjwa.

Hata hivyo, mapambano dhidi ya virusi hivyo yanasalia kuwa changamoto kubwa kwa hospitali kutokana na ukosefu wa uwezo wa kutosha, anaripoti afisa wa hospitali. Mojawapo ya mahitaji ya haraka zaidi ni uwasilishaji wa vifaa vya kinga binafsi. Na ingawa hospitali imepokea vifaa vy kwanza, ina fofu kwamba akiba inaweza kuisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *