Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka , amewataka vijana kutumia majukwaa ya vijana k…Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka , amewataka vijana kutumia majukwaa ya vijana k…

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka , amewataka vijana kutumia majukwaa ya vijana kujitambua, kuibua vipaji vyao na kuchangamkia fursa mbalimbali za kujiajiri zinazotolewa na serikali.

Akizungumza katika uzinduzi wa Jukwaa la Vijana uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Kampasi ya Mazimbu, Waziri Nanauka amesema serikali imeendelea kufanya maboresho katika mifumo ya uwezeshaji ili mikopo inayotolewa iwe rafiki, yenye tija na kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Japhar Kubecha, amewahimiza vijana kulitumia vyema jukwaa hilo kwa kujifunza, kubadilishana uzoefu na kutambua fursa zinazoweza kuchochea maendeleo yao binafsi pamoja na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Kampasi ya Mazimbu anayeshughulikia Utawala, Fedha na Mipango, Prof. Amendus Muhairwa, amesema vijana wanahitaji kupewa maarifa, ujuzi na mwelekeo sahihi wa kujiajiri badala ya kuishia kuhamasishwa kwa maneno pekee.

Naye Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Josephine Kapoma, amesema bado kuna haja kwa serikali kuendelea kuimarisha mifumo ya uwezeshaji ili vijana wengi zaidi waweze kupata mitaji na kunufaika na fursa zilizopo nchini.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *