Msewa atolewa macho na timu za UlayaMsewa atolewa macho na timu za Ulaya

HUENDA kiungo wa Kitanzania, Diana Msewa anayekipiga Trabzonspor ya Ligi ya Wanawake Uturuki akatimkia Ulaya, baada ya Kampuni yaTMJ inayowasimamia wachezaji kimataifa kuonyesha nia ya kuingia makubaliano na nyota huyo.

Mwanaspoti linafahamu kampuni hiyo ipo kwenye hatua nzuri za kufikia makubaliano na nyota huyo ambaye amekuwa na kiwango bora  tangu ajiunge na klabu hiyo msimu uliopita.

Inaelezwa kampuni hiyo ina mpango wa kumfungulia Msewa milango ya kucheza ligi kubwa zaidi Ulaya kutokana na kiwango kizuri alichoonyesha Uturuki.

Mtu wa karibu na mchezaji huyo amesema tayari kuna mazungumzo yanayoendelea na muda wowote kuanzia sasa TMJ itatangaza rasmi kuanza kufanya naye kazi.

MSE 02

“Wanaamini Diana bado ana uwezo mkubwa wa kufika mbali zaidi ya hapo alipo sasa. Ndiyo maana wameonyesha nia kubwa ya kutaka kufanya naye kazi na kumtafutia nafasi nyingine kubwa Ulaya,” amesema mtu huyo.

Chanzo hicho kiliongeza, baadhi ya timu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Hispania zimeanza kufuatilia maendeleo ya kiungo huyo jambo lililoongeza uwezekano wa kuondoka Uturuki mwishoni mwa msimu huu.

“Ofa na mawasiliano vipo mezani tayari. Kuna timu zimeanza kumuulizia na hilo limewafanya TMJ kuona ni muda sahihi wa kuingia kwenye mchakato wa kumsimamia,” kiliongeza chanzo hicho.

MSE 01

Msewa ambaye alijiunga na Trabzonspor akitokea Amed SK Women, ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi hicho kutokana na uwezo wake.

Katika msimu wake wa mwisho akiwa Amed SK Women, Msewa alifunga mabao manane na kutoa asisti nane kabla ya kuvutiwa na Trabzonspor ambayo baadaye ilimwongezea mkataba kutokana na mchango wake mkubwa katika timu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *