Ukraine: Kyiv na viunga vyake yashambuliwa vikali na Urusi, kombora la hypersonic latumikaUkraine: Kyiv na viunga vyake yashambuliwa vikali na Urusi, kombora la hypersonic latumika

Mji mkuu wa Ukraine na viunga vyake umeshambuliwa vikali na jeshi la Urusi usiku wa Jumamosi, Mei 23, kuamkia Jumapili, Mei 24, ikiwa ni pamoja na kombora la balestiki la Oreshnik, na kuua watu wasiopungua wanne. Saa chache mapema, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na Ubalozi wa Marekani huko Kyiv walielezea wasiwasi wao kuhusu uwezekano wa shambulio la Urusi lililokuwa likiandaliwa.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi Vladimir Putin aliahidi kujibu kijeshi kwa shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine kwenye majengo ya elimu katika eneo la Luhansk, linalokaliwa na Moscow, lililotokea usiku wa Alhamisi, Mei 21, kuamkia Ijumaa, Mei 22.

Kulingana na mwandishi wetu katika mji mkuu wa Ukraine, Lucas Lazo, takriban milipuko kumi mikubwa ilisikika saa 7:00 usiku, kabla ya mashamblizi zaidi kukumba jiji kutoka nchi kavu, angani, na Bahari Nyeusi. Waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP pia waliona risasi zikipita angani na kusikia milio ya bunduki aina ya rashasha, kijaribu  kuangusha ndege isiyo na rubani ikielea katikati ya jiji. Abiria waliokuwa katika kituo cha treni ya mwendo kasi katika mji mkuu wa nchi hiyo Kyiv walikuwa na wasiwasi mkubwa, mwandishi wetu anaripoti.

Moto ulikuwa bado unawaka katika baadhi ya maeneo ya makazi na viwanda Jumapili asubuhi. Mashambulizi haya ya makombora na ndege zisizo na rubani ya usiku yalisababisha vifo vya angalau watu wanne – “ikiwa ni pamoja na mtoto ambaye hana hata mwaka mmoja,” mamlaka imesema – na zaidi ya 60 walijeruhiwa, meya wa mji mkuu, Vitali Klitschko, ameandika kwenye Telegram. Ameongeza kuwa shule katika wilaya ya Shevchenkivsky pia ililengwa. Shambulio “karibu” na shule nyingine lilisababisha vifusi kuziba mlango wa makazi ambapo wakazi walikuwa wakikimbilia, ameongeza.

Kombora la masafa marefu la Oreshnik

Wakati wa shambulio hilo, jeshi la Ukraine lilionya kwenye Telegram kwamba mji mkuu ulikuwa chini ya “shambulio kubwa la makombora ya adui.” Kulingana nna jeshi hilo, karibu ndege zisizo na rubani 600 na makombora 90 yalitumika. Msemaji wa jeshi la anga pia amethibitisha leo Jumapili asubuhi kwamba kombora la Oreshnik la masafa marefu, lenye masafa ya kati na gumu sana kukatiza, lilitumika katika shambulio hilo.

Jeshi la Urusi lilipeleka Oreshnik, kombora lake jipya zaidi la hypersonic lenye uwezo wa nyuklia, mwaka jana huko Belarus, mshirika wa Moscow ambaye anashiriki mpaka na nchi tatu wanachama wa NATO na Umoja wa UlayaPoland, Lithuania, na Latvia – pamoja na Ukraine. Moscow tayari imetumia Oreshnik mara mbili tangu kuanza kwa mashambulizi yake nchini Ukraine mnamo mwezi Februari 2022.

Rais wa Urusi Vladimir Putin aliahidi jibu la kijeshi baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine usiku wa Alhamisi, Mei 21, hadi Ijumaa, Mei 22, kulenga majengo ya elimu huko Starobilsk, katika eneo la Luhansk mashariki mwa Ukraine, ambalo linakaliwa na Moscow. Shambulio hilo lilisababisha vifo vya watu wasiopungua 18 na zaidi ya 40 kujeruhiwa.

Kyiv ilikana kulenga maeneo ya raia na kudai kushambulia kitengo cha ndege zisizo na rubani za Urusi kilichokuwa katika eneo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *