
Magwiji wa soka nchini wamesifu kikosi alichookitwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Miguel Gamondi kuwa kinatengeneza wachezaji watakaotumika kwa muda mrefu Taifa Stars.
Katika kikosi hicho kinachojiandaa na mechi za kirafiki za kimataifa za kalenda ya FIFA, Gamondi amewaacha mastaa wazoefu akiwemo nahodha Mbwana Samatta(Le Havre), Shomari Kapombe, Yusuph Kagoma (Simba), Idd Nado (Azam) na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ (Yanga).
Baada ya kutangazwa kwa kikosi hicho, mtandao huu ulipata nafasi ya kuzungumza na mastaa mbalimbali kuhusu mtazamo juu kikosi hicho cha kocha Gamondi.
Staa wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, Zamoyoni Mogella amesema kwa namna alivyokiona kikosi kocha Gamondi anahitaji kuwaandaa mastaa wapya na huenda wachezaji waliyoachwa zipo sababu nyuma ya pazia.
“Mfano kama Tshabalala sijamuona katika mechi za Yanga za hivi karibuni labda ni tatizo la kiafya, ila kuhusu Kapombe pengine kocha anataka kuziandaa damu changa ingawa kiwango chake bado ni kizuri, kuhusu Kagoma na Nado siwezi kujua wana shida gani na hatuwezi kuingilia ofisi ya mtu, kikubwa Gamondi apewe muda ni kocha mzuri sana,” amesema Mogella.
Aliyekuwa beki wa Simba, Yanga na Stars, Amir Maftah amesema kwa kikosi alichokiita Gamondi anakitengeneza ili akitumie kwa muda mrefu katika michuano mbalimbali, akiamini Kapombe, Samatta, Kagoma, Tshabalala na Nado watakuwa wamepumzishwa kwa sababu tofauti na tayari ukomavu wao unajulikana.
“Jukumu la kuita wachezaji wa timu ya taifa ni la kocha mwenyewe, kikubwa tunapaswa kumuunga mkono, ingawa kuna eneo moja ninaloliona lina changamoto ni la golikipa, Simba, Yanga na Azam ndizo zenye uzoefu wa wachezaji kucheza michuano ya kimataifa, lakini wanaopata nafasi ni makipa wa kigeni katika vikosi vya timu hizo, angalau naona Manula atafanyika msaada kwa Foba na Amosi pia washambuliaji ukimuondoa Samatta anayetegemewa kwa sasa ni Mwalimu, ikitokea kaumia hakuna straika mwingine tipiko, chakufanya tubadilishe mifumo ya kuwaandaa wachezaji wa nafasi za magolikipa na mastraika tukifikilia manufaa ya taifa.”
Mtazamo wa mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ amesema:”Ninachokiona katika kikosi hicho, Gamondi ni anawaandaa wachezaji wapya ambao watatatumika kwa muda mrefu na hao wengine waliyoachwa pengine wanapumzishwa na wanasababu tofauti, namwamini ni kocha mzuri atakayeleta manufaa kwa timu yetu pia wachezaji waliyopata nafasi ni muda wao wa kupambana kuhakikisha wanakuwa mibadala mizuri wa wale ambao umri wao unawatupa mkono.”
KIKOSI KILICHOITWA
Zuber Foba, Aishi Manula (Azam), Yona Amosi(Pamba Jiji),Pascal Msindo (Azam), Nickson Kibabage(Simba),Ibrahim Hamad ‘Bacca’ (Yanga), Elias Lawi(Azam), Bakari Mwanyeto(Yanga), Vedastus Masinde (Simba), Mohamed Mussa (Mashujaa), Haji Mnoga (Salford City,Uingereza), Novatus Dismas(Coztepe FC, Uturuki),Mohammed Sagaf (Eastbourne ,Uingereza).
Wengine ni Abdukarim Kiswanya (Namungo FC),Mudathiri Yahya (Yanga),Charles M’Mombwa (Florian FC,Malta),Aphonce Mabula(Shamakhi,Azerbaidjan),Bakari Msimu (Coastal Union),Tarryn Allarakhia (Rochdale FC,Uingereza),Feisal Salum ‘Fei Toto’ (Azam), Simon Msuva(Al-Talaba, Iraq),Seleman Mwalimu(Simba),Cprian Kachwele (HFX Wanderers,Canada) na Said Khamis (Immigrations, Malaysia).
