Ebola: Visa viwili vipya vya maambukizi ya virusi vyathibitishwa nchini UgandaEbola: Visa viwili vipya vya maambukizi ya virusi vyathibitishwa nchini Uganda

Visa viwili vipya vya maambukizi ya virusi vya Ebola vimeripotiwa nchini Uganda, Wizara ya Afya ya Uganda imetangaza katika taarifa yake mnamo Mei 25, 2026.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wagonjwa hawa wawili wapya wote ni wafanyakazi wa afya katika kituo cha kibinafsi jijini Kampala, mji mkuu, wa Uganda, wizara imesema. Hii inafikisha idadi ya visa vilivyothibitishwa nchini Uganda kufikia saba tangu kuanza kwa mlipuko wa virusi vya Ebola, uliotangazwa Mei 15 katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

“Wagonjwa hao wawili wamelazwa katika kitengo cha matibabu kilichotengwa na kwa sasa wanapokea huduma. Watu wote ambao wametangamana na wagonjwa hawa  wanatambuliwa na kufuatiliwa na timu za kukabiliana na ugonjwa,” Wizara ya Afya ya Uganda imesema.

Mamlaka ya Uganda inausihi umma kuwa macho zaidi na kupendekeza kwamba mtu yeyote anayeonyesha dalili zinazoambatana na ugonjwa wa virusi vya Ebola kuripoti mara moja katika kituo cha afya kilicho karibu.

“Umma unashauriwa kuripoti mara moja mtu yeyote anayeonyesha dalili zinazoambatana na ugonjwa wa virusi vya Ebola katika kituo cha afya kilicho karibu. Ugunduzi wa mapema na matibabu huongeza kwa kiasi kikubwa nafasi ya kuishi na kusaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo,” Wizara ya Afya ya Uganda imeongeza.

Awali, Mawaziri wa Afya wa DRC, na Jamhuri ya Sudan Kusini, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa CDC Africa, Jean Kaseya, na wawakilishi kutoka WHO, UNICEF, UNFPA, na washirika wengine wa kiufundi, walipitisha mpango wa uratibu wa mpakani dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Ebola Bundibugyo unaoathiri eneo la Maziwa Makuu kwa sasa.

Hili lilikuwa jambo muhimu kutoka kwa mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri kuhusu uratibu wa mwitikio wa janga kati ya mipaka, uliofanyika Mei 22 na 23, 2026, jijini Kampala, Uganda, chini ya mada “Mshikamano wa Kikanda, Utayari, na Mwitikio Ulioratibiwa.” Washiriki walikubali kwamba ugonjwa wa virusi vya Ebola (EVD) unabaki kuwa tishio kubwa la afya ya umma, ukiwa na athari kubwa kiafya, kibinadamu, kijamii, na kiuchumi kwa nchi na eneo lililoathiriwa.

Taarifa ya pamoja iliyopitishwa inajumuisha ahadi kumi na mbili zinazolenga kuimarisha mwitikio wa mpakani dhidi ya mlipuko wa Ebola Bundibugyo. 

Kufikia Mei 15, 2026, mlipuko wa Ebola ulithibitishwa katika Mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hii ni aina adimu ya virusi ambayo hakuna chanjo au matibabu maalum.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *