Mkuu wa shirika la afya dunini WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kwamba watu zaidi ya 900 wanashukiwa kuwa wameambukizwa virusi vipya vya Ebola nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa X siku ya Jumapili, Ghebreyesus, amesema kwamba katika visa hivyo zaidi ya 900 vinavyoshukiwa, visa 101 vimethibitishwa.
Ni taarifa ambayo pia ilitolewa na wizara ya afya ya nchi hiyo kupitia mtandao wa X, ambapo wizara hiyo ilitangaza kuwa watu 119 wanashukiwa kufariki kutokana na virusi hivyo.
Siku ya Jumamosi wizara hiyo ilikuwa imetangaza maambukizi yanayoshukiwa kuwa zaidi ya zaidi ya 860 na vifo zaidi ya 200, vikirekodiwa katika majimbo matatu hasa katika jimbo la Ituri ambalo ni kitovu cha mlipuko wa virusi hivyo.
Haya yanajiri wakati huu juhudi za ufuatiliaji zikiimarishwa katika kujaribu kudhibiti msambao wa virusi hivyo ambavyo vimesababisha WHO kutangaza mlipuko huo kuwa dharura la kiafya duniani.
