
Nchini Sudan Kusini, serikali imebadilisha mkondo na kuachana na mipango ya kuondoa vifungu muhimu kutoka kwa makubaliano ya amani ya mwaka 2018. Chini ya shinikizo kutoka kwa mashirika ya kiraia na balozi nyingi za kigeni ambazo zina wasiwasi na kuanguka kwa mchakato wa amani na taasisi za mpito, marekebisho yenye utata zaidi hatimaye yameondolewa kwenye rasimu ya sheria ambayo inajadiliwa sasa Bungeni.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu akiwa Juba, Florence Miettaux
Mabadiliko ya serikali ya Sudan Kusini yalitangazwa kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri mnamo Mei 22. Rasimu ya sheria inayorekebisha makubaliano ya amani hatimaye haitapendekeza kuondolewa kwa vifungu viwili vinavyoweka nguvu ya makubaliano juu ya sheria zingine zote.
Edmund Yakani, mkurugenzi wa mashirika ya kiraia CEPO, amekaribisha “mwitikio chanya” wa serikali lakini ametoa wito wa “kujitolea kutekeleza majukumu yaliyobaki ya makubaliano ya amani.”
Makubaliano haya yaliyotiwa saini mwaka wa 2018, yanaeleza utaratibu wa uchaguzi ili kukamilisha mpito. Hata hivyo, ucheleweshaji mkubwa umesababisha serikali kutafuta njia za mkato. Muswada unaojadiliwa kwa sasa Bungeni unapendekeza kuahirishwa kwa uandishi wa katiba ya kudumu na sensa ya raia hadi baada ya uchaguzi.
Chama cha Makamu wa Rais Riek Machar, ambaye amezuiliwa na bado anakabiliwa na kesi mjini Juba, kilirud kuonyesha msimamo wake wa kukataa kwa muswada huo siku ya Jumapili, kikielezea kuhifadhiwa kwa vifungu vinavyohusu ukuu wa makubaliano ya amani kama makubaliano “ya juu”. Chama hiki cha upinzani kinadai kuondolewa kwa muswada huo na kufanyke mazungumzo “yanayojumuisha” kabla ya kuwekwa kwenye ajenda ya bunge.
