
DODOMA: WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amemteua Haji Manara kuwa msemaji wa timu zote za Taifa za Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo Mei 28, 2026, Waziri Makonda amesema Manara atafanya kazi chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na atakuwa akizisemea timu zote za Taifa za mpira wa miguu.
