Ebola DRC: Changamoto zinaendelea licha ya mgonjwa wa kwanza kupona virusi aina ya BundibugyoEbola DRC: Changamoto zinaendelea licha ya mgonjwa wa kwanza kupona virusi aina ya Bundibugyo

Mtu wa kwanza aliyekuwa ameambukizwa virusi vya Ebola (Bundibugyo) na kulazwa hospitalini, ameruhusiwa kuondoka katika kituo cha matibabu ya Ebola mnamo Mei 27 huko Rwampara, katika mkoa wa Ituri, mashariki mwa DRC. Huu ni mtu wa kupona na kuthibitishwa tangu kuzuka kwa mlipuko wa virusi vya Ebola aina ya Bundibugyo nchini DRC nahuu ni ushindi. Lakini, changamoto zinabaki kuwa kubwa. Afisa wa matibabu katika kituo hicho anaelezea hali ya kutisha. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Alifika akiwa mgonjwa. Aliondoka akiwa amepona. Kati ya hayo, kulikuwa na vipimo chanya, matibabu, huduma ya kutosha, na kisha vipimo hasi. Hakuna homa tena. Hakuna dalili tena. Milango ya kituo hicho ilifunguliwa kwa mtu huyu na akaruhusiwa kuondoka.

Lakini bila chanjo na matibabu maalum ya aina hii ya Ebola, mtu anawezaje kupona? Afisa wa matibabu katika kituo cha Rwampara anaelezea: “Kabla ya molekuli za aina ya Zaire (aina nyingine ya Ebola) kugunduliwa, watu walikuwa wakipona. Wakati mwingine, kudhibiti dalili ipasavyo kunatosha.”

Sio wagonjwa wote wanaoweza kupona kwa njia hiyo

Kuhusu kasi inayoonekana ya kupona huku, afisa wa matibabu anafafanua: “Kipindi cha ugonjwa kuweza kuthibitishwa si lazima kiwe siku 21.” Kinaanzia siku 2 hadi 21, kulingana na mfumo wa kinga wa kila mtu.

Lakini nyuma ya ushindi huu, matatizo mengine yanaendelea, kulingana na RFI. La kwanza: maabara. Sampuli nyingi hazifanyiwa vipimo. Vitendanishi vinaweza kuwepo, lakini uwezo wa kuvishughulikia bado hautoshi. Bila upimaji wa haraka, hakuwezi kuwa na ufuatiliaji wa watu waliotangamana na mgonjwa na hakutakuwa na  kuwekwa karantini mapema, na watazidi kuambukizana.

Tatizo la pili linaloendelea: mazishi. Timu haziwezi kila wakati kuendelea na zoezi hili.

Hatimaye, upinzani wa jamii unabaki kuwa mkubwa. Wale wanaofuatilia watu waliotangamana na mgonjwa hushambuliwa. Baadhi ya watu hufariki katika jamii bila kupata huduma.

Na huko Rwampara, kituo hicho bado kinafanya kazi kwa mfumo wa muda wa vitanda 19. Ujenzi wake wa kudumu unaendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *