Ebola: Vizuizi katika mpaka wa Uganda na DRC vyazua wasiwasi kwa jumuiya ya wafanyabiasharaEbola: Vizuizi katika mpaka wa Uganda na DRC vyazua wasiwasi kwa jumuiya ya wafanyabiashara

Siku moja baada ya Uganda kuchukua haua mpya katika mpaka wake na DRC katika jaribio la kudhibiti kuenea kwa mlipuko wa virusi vya Ebola, wasiwasi unaongezeka katika jumuiya ya wafanyabiashara. Kampala inasisitiza inataka kudumisha biashara, lakini chini ya udhibiti mkali wa afya. Hata hivyo, wazalishaji na wasafirishaji tayari wanahofia usumbufu wa vifaa na ucheleweshaji wa bidhaa, hasa chakula.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

DRC ni mojawapo ya masoko makuu ya usafirishaji wa Uganda. Kulingana na Chama cha Wafanyabiashara wa Uganda, mauzo ya nje kwenda Kongo yanafikia zaidi ya dola bilioni mbili kila mwaka. Mkurugenzi wake mtendaji, Ezra Muhumuza, tayari ana wasiwasi kuhusu usumbufu mkubwa katika usafiri wa mpakani, hata kama bidhaa zinaweza kuendelea kupita.

“Mpango wa kuhakikisha usalama wa malori na bidhaa zinazosafirishwa ni upi?” Tunatarajia serikali zote mbili kuzungumza na kuunda kile tunachokiita maeneo salama, ambapo madereva wanaweza kuegesha magari hadi hali itakapokuwa salama. Kwa sababu hivi sasa, huwezi kuacha malori hapo na bidhaa zinazoharibika: yana hatari ya kuchomwa moto au kuharibiwa,” anaonya.

“Kufanya biashara au kuokoa maisha?” 

Kwa baadhi ya wazalishaji, wasiwasi huu unakuja baada ya wiki kadhaa ambazo tayari zimeangaziwa na mvutano katika Mashariki ya Kati. Hata hivyo, serikali ya Uganda inasisitiza kwamba vikwazo hivi ni muhimu ili kupambana na Ebola.

“Malori bado yanatembea, lakini hakutakiwi kuwe na mikusanyiko. Madereva watakaguliwa na watalazimika kufuata hatua kali za kiafya. Wasafirishaji wenyewe lazima pia wachukue tahadhari. Ikiwa wanasafirisha bidhaa zinaweza kuharibika haraka, kwa nini wasingoje siku chache hadi hali itulie? Vizuizi hivi havitekelezwi kwa nia mbaya.” “Kitu gani kinapaswa kuwa muhimu zaidi: kufanya biashara au kuokoa maisha?” anauliza David Bahati, Waziri wa Uchukuzi wa Uganda.

Mamlaka ya Uganda inahakikisha kwamba hatua hizi zitaendelea kutumika pindi wataona hali ya kiafya bado inatia wasiwasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *