Mbunge ahoji serikali inatoa elimu bure au elimu bila adaMbunge ahoji serikali inatoa elimu bure au elimu bila ada

DODOMA;Mbunge wa Tarime Mjini, Mwita Waitara, ameuliza bungeni kama serikali inatoa elimu bure au inatoa elimu bila ada.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Dk Festus Dugange kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, amesema serikali imeendelea kutekeleza Sera ya utoaji wa ElimuMsingi bila mzazi/mlezi kuchangia ada.

”Katika kutekeleza azma hiyo, serikali ilitoa Waraka wa Elimu Na. 3 wa Mwaka 2016 kuhusu Utekelezaji wa ElimuMsingi bila Malipo, ambapo umebainisha majukumu ya kila mdau na kuweka utaratibu wa namna wanavyoweza kuchangia michango mbalimbali katika kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu katika maeneo yao.

‘’Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 hadi 2025/2026, serikali imetoa jumla ya Sh 1,394,885,918,000 kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa shule. Kati ya fedha hizo, Sh 488,190,858,000 zimetolewa kwa shule za msingi na Sh 906,695,060,000 zimetolewa kwa shule za sekondari.

‘’Utoaji wa fedha hizi umeendelea kuimarisha utekelezaji wa sera ya elimu bila malipo pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia nchini.

‘’Serikali inaendelea kusisitiza wadau wote wa elimu kuzingatia taratibu, kanuni na miongozo iliyowekwa ili kuimarisha mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji, kuongeza upatikanaji wa elimu, na kuendelea kuboresha ubora wa elimu nchini,” amesema Naibu Waziri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *