Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar ameshiriki ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 61 wa mwaka 2026 wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkutano Mkuu wa 52 wa Mwaka wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF).
Mkutano huo unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kintélé, jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo ambao kwa upande wa ujumbe wa Serikali ya Tanzania uliongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mwigulu Lameck Nchemba.
Mkutano huo wenye kauli mbiu ya ‘Kuhamasisha Ufadhili wa Maendeleo ya Afrika kwa Wingi katika Dunia Iliyogawanyika’ inayosisitiza umuhimu wa kuziba pengo la kifedha linalokua kwa mahitaji ya maendeleo ya Afrika, hasa katika mazingira ya kisiasa na kiuchumi duniani yanayobadilika kwa kasi.
Zaidi ya wajumbe 3,000 wanahudhuriwa kutoka nchi mbalimbal Afrika na Kimataifa, wakiwamo marais na wakuu wa Serikali za Afrika, mawaziri wa fedha, magavana wa mabenki kuu, washirika wa maendeleo, wawakilishi wa sekta binafsi, viongozi wa asasi za kiraia, wasomi, taasisi za utafiti, NGOs, na wadau wengine.
Upande wa Tanzania ulihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar, Dkt Hamad Omar Bakar, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali ambaye pia katika Muundo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni Gavana Mbadala wa Benki hiyo Dkt Natu El-maamry Mwamba na Kaimu Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Rished Bade.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Fedha amesema Tanzania kama ilivyo nchi nyingine inapitia changamoto kwenye eneo la miundombinu na kutaja hatua zilizopigwa katika sekta ya usafiri kupitia reli ya kisasa.
(Feed generated with FetchRSS)
