Bandari Kavu ya Azam (ICD) inatarajia kuzindua mashine ya umeme ya kubebea makasha katika kutekeleza mikakati ya matumizi ya nmishati safi na kuongeza ufanisi wa shughuli za bandarini.

Akizungumza na Azam News, Issa Jaye, Mtendaji Mkuu wa Azam ICD amesema uzinduzi huo utafanyika Juni mosi mwaka huu na utaifanya Azam ICD kuwa kampuni ya Kwanza kutumia mashine hizo hapa nchini.

Naye Carlos Li, Meneja Mkuu wa kampuni inayotengeneza mashine hizo ya Liugong Africa amesema hii inakuwa mashine ya kwanza ya umeme nchini Tanzania.

Mhariri @moseskwindi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *