Italia inalaumiwa tena kwa kumruhusu Osama Almasri Najim kukwepa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai. Kulingana na hati ya kukamatwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita, afisa huyu wa polisi wa Libya alikamatwa mapema mwaka wa 2025, kisha akaachiliwa siku mbili baadaye na kurudi Libya kwa ndege ya kijeshi ya Italia. Kufuatia kipindi hiki, malalamiko yaliwasilishwa kwa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu huko Strasbourg.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Hague, Stéphanie Maupas

Hii ni hatua nyingine ndogo tu katika kesi hii ambayo inaendelea kuaibisha Italia. Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu imeiarifu Roma kuhusu malalamiko mawili yaliyowasilishwa mwezi Februari na Aprili kwa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Binadamu huko Strasbourg na walalamikaji wawili, kufuatia kutoroka kwa Osama Almasri Najim, mkuu wa polisi wa mahakama ya Tripoli.

Walalamikaji hao wawili wanaishutumu Italia kwa ukiukaji kadhaa wa Mkataba wa Ulaya wa Haki za Binadamu, ikiwa ni pamoja na haki ya kuishi na haki ya kulindwa kutokana na mateso, unyama na udhalilishaji.

Mwathiriwa wa kwanza, mwanamke kutoka Côte d’Ivoire ambaye alikuwa bado mdogo alipofika Libya, analaani utumwa, unyanyasaji wa kingono, na mateso yaliyofanywa na wasaidizi wa Osama Almasri Najim. Hatimaye alifanikiwa kukimbilia Italia kwa kuvuka Bahari ya Mediterania mwaka wa 2017.

Mlalamikaji wa pili, mwanamume kutoka Sudan, aliondoka Sudan Kusini wakati nchi hio ilipokuwa katika vita mwaka wa 2018. Alizuiliwa Libya, katika gereza la Al-Jadida. Alilazimishwa kupigana katika kundi lenye silaha lililokuwa likiongozwa na Osama Almasri Najim.

Awali aliwasilisha malalamiko nchini Italia dhidi ya Mawaziri wa Mambo ya Ndani na Sheria, ambao walimruhusu Osama Almasri Najim kukwepa ICC. Hata hivyo, kesi yake ilifutwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *