SERENGETI BOYS: HATUTOKI MCHEZONI
Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana U17, Serengeti Boys, wameishukuru serikali kwa motisha ya shilingi milioni 500 na viwanja, wakisema imewaongezea ari na deni la kuhakikisha wanarejea kombe mkononi.
Wakizungumza na Azam Sports wakiwa mazoezini kwaajili ya maandalizi ya mchezo wa fainali, baadhi ya wachezaji na kocha mkuu wa klabu hiyo Elieneza Nsanganzelu wamesema motisha hiyo haitawatoa mchezoni na kuwafanya wabweteke badala yake imekuwa ni deni wanalopaswa kulilipa kwa Taifa.
Fainali ni Jumanne Juni 02 na utaipata LIVE #AzamSports2HD
#SerengetiBoys #AFCONU17 #LinakujaNyumbani
(Feed generated with FetchRSS)