Zaidi ya shilingi bilioni 2.6 zinatarajiwa kukusanywa katika kampeni ya GGML Kilimanjaro Challenge Against HIV/AIDS mwaka 2026, kwa lengo la kuimarisha mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini.

Kampeni hiyo imezinduliwa jijini Dar es Salaam kupitia matembezi ya pamoja na harambee, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali na wadau wa maendeleo katika kudhibiti maambukizi mapya na kupunguza vifo vinavyotokana na maambukizi ya VVU na UKIMWI.

Makamu wa Rais wa AngloGold Ashanti anayesimamia Ustahimilivu na Mahusiano Barani Afrika, Simon Shayo, amesema kampeni hiyo inalenga kusaidia huduma za kinga, matibabu na msaada kwa waathirika.

Kwa upande wake, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Susan Ngongi Namondo, amesema kupungua kwa misaada ya kimataifa kunafanya juhudi za ndani kama hizi kuwa muhimu zaidi katika kuhakikisha huduma zinaendelea kuwafikia wanaohitaji.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *