
Mwanasiasa wa Ujerumani na mbunge wa zamani wa bunge la nchi hiyo amekosoa sera za utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema: “Walowezi wa Kizayuni wanafanya ugaidi wa kimfumo dhidi ya Wapalestina, na serikali ya Ujerumani na Umoja wa Ulaya wanashiriki katika uhalifu huo kwa kunyamaza kimya.”
Jürgen Todenhofer ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba: “Israel inakusudia kuwafungia wakazi wa Gaza kwenye 30% ya ukanda wa pwani bila chakula na dawa za kutosha, na kuchukua udhibiti wa 70% iliyobaki ya eneo hilo.
Ameongeza kuwa: “Kila siku katika Ukingo wa Magharibi – ambapo kwa sasa Israel imenyakua asilimia 60 ya ardhi ya Wapalestina – walowezi wa Israel wanashambulia wakulima na wakazi wa Wapalestina, na kufanya maisha yao kuwa ya Jahanamu.”
Mbunge huyo wa zamani wa Bunge la Ujerumani ameandika: Huko Jerusalem inayokaliwa kwa mabavu, familia za Wapalestina pia mara nyingi hukabiliwa na mashambulizi ya kikatili na walowezi wa Israel.
Todenhofer ameongeza kwa kusema: “Lengo la ugaidi huu wa kimfumo unaofanywa na walowezi wa Israel ni kubadilisha maisha ya watu wa Palestina na kuyafanya kuwa ya Jahanamu, na hatimaye kunyakua ardhi yao kwa kukiuka sheria za kimataifa.”