Senegal na Ghana zimetangaza vikosi vyao vya mwisho vya wachezaji 26 kwa kila moja, tayari kwa fainali za Kombe la Dunia 2026 huko Marekani, Canada na Mexico.

Ikiwa leo Jumanne, Juni 2, 2026 ndio siku ya mwisho kwa kila timu kuwasilisha majina ya wachezaji 26 watakaoshiriki fainali hizo, wawakilishi hao wawili wa Afrika wameungana na Morocco, Afrika Kusini, Tunisia, DR Congo na Cape Verde ambazo tayari zilishakamilisha hilo.

Hakuna taarifa za kushtukiza za kuachwa kwa baadhi ya mastaa katika vikosi hivyo vya Ghana na Senegal kutoka katika vikosi vyao vya awali ambavyo vilitangazwa wiki kadhaa zilizopita.

Kocha Mkuu wa Senegal, Pape Thiaw, amewaacha wachezaji wawili tu kutoka katika kikosi chake cha awali cha wachezaji 28 kilichotangazwa Mei 21 mwaka huu.

Walioachwa na Thiaw, wote ni mabeki ambao ni Moustapha Mbow wa Paris FC na beki wa Anderlecht ya Ubelgiji, Ilay Camara.

Waliopewa uhakika wa kuwepo Kombe la Dunia ni makipa Edouard Mendy, Mory Diaw na Yehvann Diouf huku mabeki wakiwa ni Krepin Diatta, Antoine Mendy, Kalidou Koulibaly, El Hadji Malick Diouf, Mamadou Sarr, Moussa Niakhate, Abdoulaye Seck na Ismail Jakobs.

Wachezaji wa nafasi ya kiungo walioitwa ni Idrissa Gueye, Pape Gueye, Lamine Camara, Habib Camara, Pathe Ciss, Pape Matar Sarr na Bara Ndiaye.

Washambuliaji walioitwa ni Sadio Mane, Ismaila Sarr, Iliman Ndiaye, Assane Diop, Ibrahim Mbaye, Nicolas Jackson, Bamba Dieng na Cherif Ndiaye.

Kwa upande wa Ghana, Kocha Carlos Queiroz amepunguza wachezaji wawili katika kikosi chake cha awali na kubaki na wachezaji 26 atakaoenda nao Kombe la Dunia.

Walioachwa ni kipa Solomon Agbasi na beki Paul Reverson.

Majeraha ya beki Alexander Djiku yamemfanya kocha Queiroz amuondoe kikosini na nafasi yake itazibwa na Derrick Luckassen.

Kikosi cha wachezaji 26 wa Ghana watakaoshiriki Kombe la Dunia ni makipa Benjamin Asare, Lawrence Ati-Zigi, Joseph Anang na mabeki ni Baba Abdul Rahman, Gideon Mensah, Marvin Senaya, Alidu Seidu, Abdul Mumin, Jerome Opoku, Jonas Adjetey, Kojo Oppong Peprah na Derrick Luckassen.

Viungo ni Elisha Owusu, Thomas Partey, Kwasi Sibo, Augustine Boakye, Caleb Yirenkyi, Abdul Fatawu Issahaku na Kamal Deen Sulemana

Washambuliaji ni Christopher Bonsu Baah, Ernest Nuamah, Antoine Semenyo, Brandon Thomas-Asante, Prince Kwabena Adu, Inaki Williams na Jordan Ayew.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *