.

Chanzo cha picha, X/US Central Command

Jeshi la
Marekani linasema limeanzisha mashambulizi ya “kujilinda” dhidi ya
Iran na kudungua makombora ya masafa marefu na ndege zisizo na rubani kwenye
meli na nchi za Ghuba.

Mashambulizi
hayo kwenye Kisiwa cha Qeshm, katika Mlango-Bahari wa Hormuz, yalikuwa “kujibu majaribio ya mashambulizi ya Iran kote Mashariki ya Kati”,
Kamandi Kuu ya Marekani (Centcom) ilisema.

Iran ilisema
imeshambulia kambi na helikopta za Marekani katika “nchi ya kikanda”
kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani kama kulipiza kisasi.

Centcom
ilisema Tehran imerusha makombora mawili dhidi ya Kuwait na matatu dhidi ya
Bahrain, ambayo yote yalivunjika vipande vipande au kuzuiliwa.

Mashambulizi
ya hivi karibuni yanatokea huku mazungumzo ya kusitisha mapigano yakikwama,
baada ya mazungumzo kuhusu makubaliano ya kukomesha vita vyao vya miezi kadhaa
kushindwa kuendelea mwishoni mwa juma.

Centcom
iliongeza kuwa shambulio hilo katika Kisiwa cha Qeshm lilikuwa limelenga kituo
cha udhibiti wa ardhini cha jeshi la Iran, na kwamba jeshi la Marekani pia
lilidungua ndege tatu zisizo na rubani ambazo zilikuwa zimerushwa na Iran
kuelekea kwa “mabaharia raia waliokuwa wakipitia maji ya kikanda kihalali”.

IRGC ilisema “kuvuruga usalama wa Mlango-Bahari wa Hormuz kutakuwa na gharama kubwa kwa
jeshi la Marekani lenye uchokozi”.

Iran imekuwa
ikishambulia mara kwa mara maeneo ya Bahrain na Kuwait, ambapo kambi za kijeshi
za Marekani zipo.

Hapo awali,
Centcom ilisema imeishambulia na kuiharibu meli ya mafuta isiyo na mizigo
iliyokuwa ikielekea Iran, kama sehemu ya kizuizi cha majini cha Washington
kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *