Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa leo katika mtandao wa X, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), limeeleza wasafiri wote wanaoingia au kutoka nchini wanatakiwa kujaza fomu ya taarifa za msafiri na kufanyiwa uchunguzi wa afya kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari zao.

Mapema wiki hii, Wizara ya Afya ya Uganda, kwa ushirikiano na WHO na wadau wengine wa afya, ilifanya tathmini ya utaratibu wa uchunguzi wa wasafiri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe. Uwanja huo hupokea maelfu ya wasafiri kila siku, huku uchunguzi ukijumuisha tathmini ya uwezekano wa kuathiriwa na ugonjwa, upimaji wa joto la mwili na, iwapo msafiri atabainika kuwa na homa, kufanyiwa tathmini ya kina ya hatari ya Ebola na wahudumu wa afya waliopewa mafunzo maalumu.

Mamlaka za afya zimesema kuwa hatua hizo za ufuatiliaji zimeimarishwa ili kuzuia kuenea kwa Ebola na kuhakikisha wagonjwa wanaoweza kuwa na maambukizi wanagunduliwa mapema katika maeneo muhimu ya kuingia na kutoka nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *