
Wakati FIFA ikithibitisha namba ya wachezaji 1,248 kutumika na vikosi vya timu 48 katika Kombe la Dunia mwaka huu, thamani ya jumla ya vikosi vya timu saba inaweza kujenga viwanja sita vya soka vyenye hadhi ya kisasa kama unaojengwa Arusha Tanzania kwa ajili ya kutumika kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Uwanja wa soka Arusha unajengwa kwa gharama ya Sh338.54 milioni na unategemewa kuchukua idadi ya mashabiki 30,000.
Tathmini ya mtandao wa Transfermkt ya thamani za vikosi iliyofanywa kwa timu 48 zinazoshiriki Kombe la Dunia inaonyesha kuwa jumla thamani ya jumla ya vikosi vya Ufaransa, Hispania, England, Ujerumani, Uholanzi, Brazil na Ureno, inaweza kugharamia ujenzi wa viwanja kama ule wa Arusha sita na chenji ikabakia.
Gharama ya ujenzi wa Uwanja wa Arusha ni Sh338.54 na kujenga viwanja sita kama hivyo, kiasi cha fedha kinachohitajika ni Sh2 trilioni.
Vikosi vya timu hizo saba vina thamani ya Sh2.14 trilioni ambayo ni Sh1.4 trilioni zaidi ya gharama za ujenzi wa viwanja sita vya kisasa vya soka ambavyo kila kimoja kinaweza kuingiza mashabiki 30,000.
Katika vikosi hivyo, Ufaransa ndio kinara kwa kuwa na kikosi chenye thamani kubwa zaidi ambapo kina thamani ya Sh4.6 trilioni.
Nafasi ya pili inashikiliwa na kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi ambacho kina thamani ya Sh3.9 trilioni.
Hispania yenye kikosi chenye thamani ya Sh3.8 trilioni inashika nafasi ya tatu na inayoshika nafasi ya nne ni Ureno ambayo kikosi chao kina thamani ya Sh3.1 trilioni.
Katika orodha hiyo, nafasi ya tano ipo Ujerumani ambayo kikosi chake kina thamani ya Sh3 trilioni na nafasi ya sita ipo Brazil na kikosi chake chenye thamani ya Sh2.8 trilioni.
Timu inayoshika nafasi ya saba kwa kuwa na kikosi chenye thamani kubwa katika Kombe la Dunia ni Uholanzi ambayo kikosi chake kina thamani ya Sh2.6 trilioni.