
Nchi zitakazochaguliwa ni Austria, Ureno, Zimbabwe, Trinidad na Tobago ingawa upigaji kura unaendelea kwa kiti kimoja kilichobaki cha Mataifa ya Asia-Pasifiki.
Nchi hizi zilizochaguliwa zitahudumu kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe 1 Januari 2027 hadi 31 Desemba 2028, na zimechukua nafasi za Somalia, Pakistan, Panama, Denmark na Ugiriki, ambazo mihula yao itaisha mwishoni mwa mwaka huu 2026.
Nchi zilizochaguliwa ni
Makundi ya Kikanda
Jumla ya nchi saba zilikuwa zimewania nafasi tano katika makundi mbalimbali ya kikanda. Austria, Ujerumani na Ureno zinashindania nafasi mbili zilizotengwa kwa Kundi la Mataifa ya Ulaya Magharibi na Nchi Nyingine (WEOG), huku Kyrgyzstan na Ufilipino zikishindania nafasi moja iliyotengwa kwa Kundi la Asia na Pasifiki.
Katika makundi ya Afrika na Amerika ya Kusini pamoja na Karibe, Zimbabwe na Trinidad na Tobago zimegombea bila wapinzani. Hali hiyo ilifanya mijadala na ushindani mkubwa kuelekezwa katika makundi ya Ulaya Magharibi na Asia-Pasifiki, ambako nchi kadhaa ziliwania nafasi chache zilizopo.
Mara ya kwanza
Uchaguzi huu una umuhimu wa kipekee kwa Kyrgyzstan, ambayo haijawahi kuwa mwanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ikiwa itachaguliwa, itakuwa mara ya kwanza kwa taifa hilo la Asia ya Kati kuhudumu katika chombo hicho chenye jukumu la msingi la kudumisha amani na usalama wa kimataifa. Ufilipino nayo inalenga kurejea katika Baraza hilo baada ya kuhudumu katika vipindi vya awali.
Baraza la Usalama lina jumla ya wanachama 15, wakiwemo wanachama watano wa kudumu na wanachama 10 wasio wa kudumu wanaochaguliwa na Baraza Kuu kwa mihula ya miaka miwili inayopishana. Uchaguzi hufanyika kila mwaka ili kujaza nafasi za wanachama watano wanaomaliza muda wao wa kuhudumu, hatua inayolenga kuhakikisha uwakilishi wa kikanda na mwendelezo wa kazi za Baraza katika kudumisha amani na usalama duniani.