Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) limetoa wito kwa wananchi hasusan vijana, kuzitumia taka kama fursa ya kiuchumi, kwa kuzitenganisha na kuzirejeleza kwa lengo la kupata bidhaa mbalimbali.
Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Meneja wa (NEMC) Kanda ya Kati Bw. NOVATUS MUSHI, kwenye maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
Pamoja na Kueleza ni kwa namna gani Baraza hilo limefanikiwa kupanda miti takribani 40,000 nchi nzima, kwenye maadhimisho ya miaka 40 toka baraza hilo lianzishwe, Meneja huyo wa NEMC akachukua nafasi hiyo kueleza ni kwa namna gani sasa wameamua kuwekeza katika teknolojia, ili kusimamia mazingira kwenye uweledi wa hali ya juu.
(Feed generated with FetchRSS)