
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa usiku wa Jumatano, Juni 3, kuamkia Alhamisi, Juni 4, Israel na Lebanon zimetangaza makubaliano yao ya kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano na kuanzisha maeneo ya majaribio chini ya udhibiti wa jeshi la Lebanon. Nchi hizo mbili pia zitashiriki katika mazungumzo mapya katika wiki ya Juni 22.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Usiku wa Juni 3 kuamkia Juni 4, Israel na Lebanon zimetangaza kuwa zimekubaliana kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano, kuanzisha maeneo ya majaribio chini ya udhibiti wa jeshi la Lebanon, na kushiriki katika mazungumzo mapya katika wiki ya Juni 22, kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya siku mbili za mazungumzo huko Washington.
“Kufuatia mazungumzo yaliyofanywa chini ya usimamizi wa Marekani, Israel na Lebanon zimekubaliana kutekeleza makubaliano ya kusitisha mapigano,” ambayo yatategemea “kusitishwa kabisa kwa mapigano ya Hezbollah na kuwaondoa wanachama wote wa Hezbollah kutoka eneo la Kusini mwa Litani,” kulingana na taarifa iliyosainiwa na pande tatu katika mazungumzo hayo.
Israel na Lebanon pia zimekubaliana kushiriki katika duru mpya ya mazungumzo katika wiki ya Juni 22 kwa lengo la kufikia “makubaliano kamili,” taarifa hiyo inaongeza.
Pande hizo mbili zinafikia katika hatua hii baada ya mashambulizi ya Israel kuua watu wasiopungua tisa kusini mwa Lebanon siku ya Jumatano na Hezbollah kufyatua makombora kaskazini mwa Israel.
“Nchi zote zilithibitisha tena kwamba mustakabali wa uhusiano kati ya Israeli na Lebanon lazima uamuliwe na serikali mbili huru. Zilikataa jaribio lolote, la serikali yoyote au mhusika yeyote asiye wa serikali, kushikilia siku zijazo za Lebanon,” ilisema taarifa hiyo.
Makubaliano hayo pia yanategemea “kuwahamisha wanajeshi wote wa [Hezbollah]” kutoka eneo ambalo Israeli inadhibiti kusini mwa Lebanon kutoka mto Litani hadi mpakani.
Nchi hizo mbili zitakutana tena tarehe 22 Juni kufanya mazungumzo zaidi “kwa lengo la kufikia makubaliano kamili”. Hezbollah bado haijatoa maoni hadharani kuhusu tangazo hilo.