Katika ripoti yake mpya yenye kichwa “Nafuu Zaidi, Safi Zaidi, Haiwezi Kuzuilika, Teknolojia Safi Zinazoleta Matokeo kwa Ajili ya Tabianchi“, UNEP imeeleza kuwa baadhi ya teknolojia rafiki kwa mazingira zinaelekea kufikia hatua ambapo matumizi yake yataenea kwa kasi na kusaidia kupunguza utegemezi wa mafuta ya kisukuku.

Ninaamini sasa tunafikia hatua ambapo tunaweza kuvunja utegemezi mkubwa wa makaa ya mawe, mafuta na gesi,” amesema Anne Olhoff, Mkurugenzi wa Kituo cha UNEP cha Tabianchi mjini Copenhagen.

Nishati mbadala ndiyo chaguo la bei nafuu zaidi

UNEP imesema gharama za nishati ya jua na upepo zimepungua kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni, na kufanya nishati mbadala kuwa chaguo la bei nafuu katika maeneo mengi duniani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, magari ya umeme sasa yanachangia zaidi ya robo ya mauzo ya magari mapya duniani, yakichochewa na kushuka kwa gharama za betri na kuongezeka kwa miundombinu ya kuchaji.

UNEP pia imeeleza kuwa usanifu bora wa majengo, unaotumia vivuli na uingizaji hewa wa asili, unaweza kupunguza joto la ndani na kupunguza matumizi ya nishati ya viyoyozi vya kupooza majengo.

© Unsplash/Sergei A Mifumo ya kupoeza ni mchangiaji mkubwa wa mabadiliko ya hali ya hewa.

Pampu za joto zatoa suluhisho

Ripoti hiyo pia imebainisha kuwa pampu za joto zinasaidia kupunguza matumizi ya nishati katika kupasha na kupooza majengo, jambo linaloweza kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.

Kwa mujibu wa UNEP kupunguza upotevu wa chakula ni moja ya njia za haraka na nafuu za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu huku ikiimarisha uhakika wa chakula.

Shirika hilo limesisitiza kuwa mafanikio ya teknolojia hizi yanategemea uwekezaji, sera thabiti na uungwaji mkono wa umma ili kusaidia dunia kufikia malengo ya tabianchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *