Vance

Chanzo cha picha, Getty Images

Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance, amesema kwamba Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, “bila shaka amekosea katika baadhi ya mambo”, huku uhusiano kati ya washirika hao wawili katika vita dhidi ya Iran ukionekana kuwa na msukosuko katika wiki za hivi karibuni.

Ingawa Vance hakutoa mifano maalumu, aliiambia CBS News kwamba Netanyahu “anapigania kwa nguvu maslahi ya nchi yake”, lakini maslahi hayo si mara zote yanalingana na yale ya Marekani.

Kauli zake zinaashiria waziwazi zaidi kwamba uhusiano kati ya washirika hao wa muda mrefu umekuwa ukikabiliwa na changamoto hivi karibuni.

Hivi karibuni, Rais wa Marekani Donald Trump anaripotiwa kutofautiana na Netanyahu kuhusu hatua za kijeshi za Israel nchini Lebanon, ambazo zilisababisha mashambulizi mapya na kutishia juhudi za mazungumzo ya amani na Iran.

Marekani na Iran zilirushiana mashambulizi kwa siku ya pili mfululizo usiku kucha, jambo lililoongeza shinikizo kwenye makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokuwepo tangu mwezi Aprili.

Hali hiyo ilikuja baada ya Trump kusema kwamba Tehran ilikuwa imechukua “muda mrefu sana kufikia makubaliano” ya kumaliza vita. Hata hivyo, kuongezeka kwa mapigano kulichochewa na matukio nchini Lebanon, ambako Israel imeendelea na operesheni dhidi ya Hezbollah, kundi linaloungwa mkono na Iran.

Wiki iliyopita, Trump alimwambia mwandishi wa habari wa Axios kwamba alimwita Netanyahu “mwendawazimu kabisa” katika mazungumzo ya simu, akisema alikuwa amekerwa na “kupigana kwake mara kwa mara na Lebanon.”

Katika mahojiano yanayotarajiwa kurushwa hewani Jumapili, Vance alisema:

“Waziri Mkuu Netanyahu, anaongoza nchi ambayo kwa hakika imekuwa mshirika wa karibu sana wa Marekani.”

Hata hivyo, aliongeza kuwa Marekani na Israel si lazima zikubaliane katika kila suala la sera au hatua za kijeshi, licha ya ushirikiano wao wa muda mrefu.

Unaweza kusoma;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *